Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau kiduchu waipokea Stars

80890 Pic+stars Wadau kiduchu waipokea Stars

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MAKUMI  ya wadau wa soka wamefika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal Three kwa ajili ya kuipokea timu ya Taifa Stars. Mapokezi hayo ni baada ya kufuzu kucheza fainali za CHAN zinazotarajiwa kufanyika nchini Cameroon mwakani. Taifa Stars imeiondosha Sudan katika fainali hizo kwa faida ya bao la ugenini baada ya kufungwa nyumbani 1-0 na wameshinda ugenini 2-1. Idadi ya wadau hao waliojitokeza uwanjani si wengi kama ilivyokuwa miaka 10 iliyopita chini ya Kocha Mbrazil, Marcio Maximo. Stars ilipokelewa kama hivi baada ya kuitoa Sudan, kulikuwa na gari maalumu la wachezaji,  mashabiki wengi katika magari tofauti walizunguka Jiji zima la Dar es Salaam. Wadau hao wa soka wameungana na viongozi mbalimbali wa soka Tanzania kama Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),  Wallace Karia,  Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mng'uto na Katibu wa TFF, Wilfred Kidao. VIKUNDI VYA USHANGILIAJI Nje ya uwanja wa ndege kuna kikundi cha ushangiliaji kinaimba na kucheza ngoma za shangwe Mambo yote hayo ni katika kuisubiri kuishangilia Stars ambayo mpaka majira ya saa 12:55 walikuwa hawajatoka nje.

Chanzo: mwananchi.co.tz