Kikosi cha vinara wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Yanga SC kinaondoka leo Dar es salaam kueleka Mkoani Lindi ambako watacheza mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC Jumamosi November 20 katika Dimba la Ilulu ikiwa ni mchezo wa raundi ya sita.
Kikosi cha Yanga kitaondoka na wachezaji 23 kueleka katika mchezo huo, na ni wachezaji watano wa kikosi hicho ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi kinachosafiri leo ambao ni Yacuba Sogne, Balama Mapinduzi, Dickson Ambundo, na Ramadhani Kabwili hawa wote wanakosekana kutokana na kuwa majeruhi lakini mchezaji Ditram Nchimbi anakosekana kutokana na mambo ya kifamilia.
Timu hiyo ya Wanchi itakuwa na michezo miwili mfululizo ya ugenini, Juamamosi Novemba 20 watacheza na Namungo Saa 10:00 Jioni katika Dimba la Ilulu, baada ya mchezo huo watasafiri mpka Jijini Mbeya ambako watacheza dhidi ya Mbeya Kwanza Novemba 30, 2021. Baada ya michezo hiyo Kikosi hicho kitarejea Dar es salaam kucheza mchezo wa Dabi ya Kariakaoo dhidi ya watani zao Simba SC Disemba 11, 2021.
Yanga ni timu pekee iliyoshinda michezo yote mitano (5) ya Ligi Kuu wakiwa wanaongoza ligi kwa alama 15 tofauti ya alama nne (4) dhidi ya Simba SC wanoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 11.