Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji wa timu ya Mwena FC, Mtwara wapata ajali

7450 Wachezaji.png TZW

Fri, 4 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Wachezaji wa klabu ya Mwena FC ya wilayani Masasi mkoani Mtwara wamepata ajali ya gari maeneo ya kijiji cha Chikupwe na kupoteza viongozi wake wawili wakati wakitokea Newala kwenye mchezo wa kirafiki kujiandaa na michuano ya mabingwa wa Mkoa inayotarajia kuanza wikiendi hii.



Afisa habari wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Mtwara (MTWAREFA), Juma Mohamed ameelezea hali ya ajali hiyo ilivyotokea.

Walienda Newala kucheza mchezo wao wa mwisho wa kujipima nguvu kabla ya kuondoka kuelekea Singida ambapo ndiyo kituo chao cha mashindano, wakati wanarudi ilikuwa ni majira ya saa 3 usiku walipofika kwenye kijiji cha Chikupwe wilayani Masasi gari yao ikapata pancha.

Wakaegeshe gari pembeni na kuteremka wachezaji na baadhi ya viongozi waliyokuwa wameambatana na timu kwaajili ya matengenezo ya tairi ili waendelee na safari ilikuwa inaelekea Mwena ambapo ndiyo maskani yake.

Wakati wanaendelea na ukarabati wa tairi ndipo ikatokea Rover4 ilikuwa inapita ilikuwa spidi sana ndipo ikaweza kuwavaa pale walipokuwa wanafanya matengenezo.

Baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wameiomba TFF kuiyongezea muda timu hiyo kwakuwa ipo kwenye kipindi kigumu.

Tatizo lililotukuta ni kubwa kwakuwa timu imepoteza baadhi ya watu wake muhimu na baadhi ya wachezaji wapo majeruhi tunaiyomba TFF na waandaji wa mashindano kuiyongezea muda kidogo na kutubadilishia ratiba.  Jafari Lionge Mwenyekiti chama cha soka Masasi.

Kamanda wa polisi mkoani Mtwara, Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, timu ya Mwena FC ni mabingwa wa mkoa Mtwara ambao wanataria kushiriki michuano ya mabingwa wikiendi hii.

Loading...
Chanzo: bongo5.com