Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Young Africans walamba milioni 500

WhatsApp Image 2021 07 05 At 16.51.03.jpeg Wachezaji Young Africans walamba milioni 500

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: dar24.com

Mfadhili wa klabu ya Young Africans Ghalib Salim Mohamed ‘GSM’ ameripotiwa kutoa Shilingi milioni 500 kwa wachezaji wa klabu hiyo, baada ya kuibanjua Simba SC juzi Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

GSM ameripotiwa kutoa zawadi hiyo, kama kutimiza ahadi yake kwa wachezaji wa Young Africans ambao alikutana nao kabla ya kukutana na Simba SC, na kuwaahidi endapo watashinda atawapatia kiasi hicho cha pesa.

Taarifa kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo ni kwamba hawakutaka kupishana na fedha hizo na kwamba walitambua viongozi wao wanataka ushindi nao wakafanya kweli.

Simba SC yaivutia kasi KMC FCHesabu za harakaharaka ni kwamba kuna uhakika kila mchezaji haitapungua kiasi cha Shilingi milioni 20 katika ahadi hiyo ya vigogo wa klabu yao.

Ahadi hiyo inaweza kuwashtua wengi kutokana kuwa ndio ahadi kubwa kwani hakuna klabu imewahi kutoa ahadi kubwa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara zaidi ya hiyo kwa msimu huu 2020/21.

Prince Dube hatarini kuikosa Simba SCBao la ushindi la Young Africans katika mchezo wa Jumamosi (Julai 03) lilifungwa na kiungo mzawa Zawadi Mauya dakika ya 11, kwa kupiga shuti kali lililombabatiza beki wa pembeni wa Simba SC Shomari Kapombe.

Ushindi huo umeiwezesha Young Africans kufikisha alama 70, huku ikisalia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Simba SC ikiwa kileleni kwa kumiliki alama 73.

Chanzo: dar24.com