Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Yanga wajazwa mamilioni

11624 Pic+yangazzz TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Morali ya wachezaji wa Yanga imepanda baada ya vigogo wa klabu hiyo kuwasili mkoani hapa wakitanguliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Hussein Nyika.

Muda mfupi baada ya kuwasili kambini, Nyika alitoa fedha kwa wachezaji baada ya kuhudhuria mazoezi ya kikosi hicho.

Kigogo huyo ameongozana na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omari Kaya ambao baada ya mazoezi kumalizika walizungumza na wachezaji.

Baada ya mazungumzo hayo Nyika alimkabidhi fedha meneja wa Nadir Haroub ‘Cannavaro na mratibu wa klabu hiyo Hafidh Saleh.

Awali, mmoja wa mabosi wa Yanga alitangulia kutuma fedha kwa wachezaji kabla ya ujio wa Nyika hatua iliyoamsha morali ya wachezaji.

Mmoja wa wachezaji (jina tunalo) aliliambia gazeti hili fedha hizo ni posho kutoka kwa mabosi na uongozi wa Yanga baada ya kuvutiwa na nidhamu, kujituma wakiwa kambini.

“Viongozi wametupa posho kidogo kocha alikuwa anawaambia watu wanavyojituma na wao waliona watupe fedha hizo,”alisema mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi.

Chanzo: mwananchi.co.tz