Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Stars wakunwa udhamini wa Serengeti Premium Lager

TAIFA Wachezaji Stars wakunwa udhamini wa Serengeti Premium Lager

Thu, 9 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Timu ya Taifa, (Taifa Stars), wameeleza kuwa siri ya mafanikio yao ya kufuzu kucheza Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka jana ni kutokana na udhamini wa Bia ya Serengeti Premium Lager na kusema udhamini huo umekuwa chachu kubwa kwa mafanikio katika michezo yao.

Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Bocco amesema udhamini wa Bia ya Serengeti umeiwezesha timu kupiga hatua kubwa ikiwa ni pamoja na kufuzu kucheza Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka jana, baada ya miaka 39 tangu ifuzu mara ya mwisho.

“Mpira unahitaji uwekezaji ili kupata mafanikio. Kampuni ya bia ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti imeweza kutoa udhamini ambao umekuwa chachu kubwa katika kuiimarisha timu yetu ya taifa. Pengine kama siyo udhamini huu tusingeweza kufika hapa tulipofika leo,” amesema Bocco.

Kampuni ya SBL kupitia Bia ya Serengeti ilikuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa kuanzia mwaka 2017 baada kusaini mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa nchini (TFF).

Naye kiungo wa timu hiyo, Frank Domayo amesema kupitia udhamini huo pia wamefanikiwa kujenga umoja na uzalendo kwa mashabiki wa soka jambo ambali limekuwa likiwapa hamasa kubwa wachezaji kufanya vizuri katika michezo yao.

“Mdhami amefanya kazi kubwa kuwaleta Watanzania pamoja na kuhamasisha uzalendo kwa timu yao ya taifa kupitia vyombo vya habari na kampeni zinazowahusisha wachezaji moja kwa moja,” amesema

Frank Domayo.

Kwa upande mwingine Domayo amesema mdhamini amekuwa akifanikisha maandalizi mazuri kwa kuhakikisha kuwa mahitaji ya wachezaji na timu kwa ujumla yanapatikana kwa uhakika na kwa wakati pia.

‘Tumeona tofauti kubwa wakati bia ya Serengeti ikiwa mdhamini wa timu yetu ya taifa. Tumekuwa tukikaa kwenye hoteli nzuri tunaposafiri na tunapokuwa kambini na hata maslahi yetu sisi wachezaji yameboreshwa kwa kiasi kikubwa jambo ambalo limetufanya tujitume zaidi,” amesema Beki wa kulia wa timu hiyo Erasto Nyoni, amesema mdhamini kwa kiasi kikubwa amekuwa karibu na wachezaji jambo ambalo limekuwa likiwatia moyo. Mdhamini amekuwa na timu siyo tu ndani ya uwanja bali hata nje ya uwanja kwa kutupa hamasa na hili limekuwa likiwajenga vyema wachezaji kisaikolojia,”.

Naye mlinda mlango wa timu hiyo Mechata Mnata amesema mdhamini amekuwa akijitahidi kuipa timu kila aina ya ushirikiano na hivyo kufanya maandalizi yawe mazuri na kuweza kufanya vizuri katika mechi zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live