SIKU moja baada ya kutolewa kwa taarifa ya kuondoka kwa Herritier Makambo katika klabu ya Yanga baada ya kupata timu nyingine ya kuitumikia msimu ujao wadau wamefunguka kuwa ni wakati sahihi kwa mchezaji lakini klabu itakuwa na kasi kubwa ya kuziba bengo lake.
Imeelezwa kuwa Makambo ameingia mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Horoya ya Guinea na ameachana na Yanga akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja baada ya kusajili miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu.
Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti walisema Makambo alitua Yanga akiwa hayupo katika hari nzuri ya kiushindani ilichukua muda hadi mashabiki wakamuelewa na anaondoka wakati ambao ni muhimu kikosini na yupo katika nafasi nzuri ya kuipa matokeo timu.
Mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Mayai alisema mkataba wake unakipengere ambacho kinamruhusu kuondoka muda wowote endapo akipata timu ya kuchezea hivyo ni muda wake kuondoka japo anaacha pengo kubwa katika klabu hiyo.
"Nafikiri kwa asilimia kubwa ya wachezaji wanaotoka Congo mikataba yao inavipengere kama hivyo sasa ni muda wa viongozi kujua namna ya kutengeneza plani B kwa nyota wao wenye mikataba yenye vipengere kama ivyo ili kuweza kunufaika kwa kuwamiliki muda wanaoutaka na kuwa na maamuzi ya kuwauza au kuto kuwauza,"
"Makambo ni mchezaji muhimu katika klabu ya Yanga amekuwa akiipa timu matopkeo katika michezo muhimu kitu kizuri kwa Yanga wanamkosa msimu ukiwa mwishoni japo bado watakuwa na mtihani wa kufanya kuhakikisha wanampata mchezaji mwingine ambaye ataingia haraka katika mfumo wao," alisema.
Kocha wa zamani wa klabu hiyo Kenny Mwaisabula 'Mzazi' amesema ni muda sahihi kwa mchezaji kuondoka kutokana na kikubwa alichokifanya ndani ya klabu yake hiyo na kuwashawishi wawekezaji wengine lakini kwa klabu kaacha pengo ambalo litachukua muda mrefu kuliziba.
"Makambo hakukubalika mapema ndani ya Yanga lakini baadaye alijitengenezea ufalme na kuonekana ndio mchezaji tegemeo kaondoka akiwa ameisaidia timu kupata matokeo na kuweza kuwa katika nafasi nzuri kwenye msimamo pamoja na chgangamoto walizokuwa wanazipitia," alisema