Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabrazili Simba wamshika Aussems

73792 Wabrazili+pic

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WACHEZAJI wawili wapya Wabrazili katika kikosi cha Simba Tairone Zaguiero na Gerson Fraga walitumika kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza kwenye mechi ya kimashindano dhidi ya JKT Tanzania waliyoshinda 3-1.

Katika mchezo huo Zagueiro alicheza beki wa kati kutokana na kukosekana kwa Pascal Wawa ambaye alikuwa majeruhi na ndio amekuwa akicheza mara kwa mara katika nafasi hiyo tangu msimu uliopita.

Zaguiero alionekana kucheza kwa kuelewana na beki mwenzake wa kati Erasto Nyoni, kwa kuwazuia washambuliaji wa JKT Tanzania Daniel Lyanga na Hassan Mwaterema, ambao walishindwa kuonesha makali yao.

Fraga alicheza katika nafasi ya kiungo mkabaji kutokana hakuwepo Jonas Mkude, ambaye anaumwa na ndio hutumika mara kwa mara katika kikosi hiko kama ilivyokuwa katika mechi tatu za kimashindano ambazo wamecheza msimu huu dhidi ya UD Songo mbili na Azam.

Kocha wa Simba Patrick Aussems, alisema siku zote huwa wanauliziwa wachezaji hao Wabrazili Zaguiero na Fraga na kile ambacho walikionesha katika dakika zote tisini ndio alikuwa akizungumza kabla ya kuanza kuwatumia.

Alisema walikuwa wakiuliziwa siku nyingi na watu wengi walitamani kuwaona wakicheza na kwake wamefanya vizuri kwa kila mmoja kutokana na majukumu yake aliyowapatia ndio maana walimaliza dakika zote za mchezo.

Pia Soma

Advertisement   ?
“Nawaona watakuja kufanya vizuri zaidi kwani mechi bado nyingi na wana nafasi ya kutumika na kucheza ndani ya timu kijumla wote walikwenda kutimiza majukumu ya kazi ambayo ilikuwa inatakiwa ifanywe na wao,” alisema.

“Mabadiliko ya kikosi yamefanyika kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi lakini nina kundi la wachezaji 30, ambao wote nawaamini na nitawapa nafasi ya kuipigania timu kila mmoja kulingana na mchezo wenyewe husika,” alisema Aussems.

MSIKIE MILAMBO

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ua umri wa miaka 17, Serengeti Boys Oscar Milambo, alisema amewafatilia Wabrazili hao Zagueiro na Fraga katika mechi yao ya kwanza ya kimashindano na kila mmoja alifanya vizuri kwa nafasi yake.

Mlambo alisema Zaguiero alicheza kwa kuelewana na Nyoni, huku akionyesha umahiri katika kukaba na kuzuia mashambulizi kwa timu pinzani, lakini amekuwa akianzisha mashambulizi na kupiga pasi ndefu na fupi ambazo zilikuwa zinafika kwa mlengwa.

Kwa upande wa Fraga anatakiwa kuzoea mazingira zaidi na kupata muda wa kucheza mechi nyingi za ushindani zenye nguvu ili kuweza kuwa sawa na wenzake kwani ameonekana kucheza mpira mzuri wa kuelekezwa lakini ni mzuri katika matumizi ya nguvu.

Chanzo: mwananchi.co.tz