Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wababe wa Simba, Azam wachezea vichapo Kombe la Shirikisho Afrika

82033 Pic+udsongo Wababe wa Simba, Azam wachezea vichapo Kombe la Shirikisho Afrika

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Wababe wa Simba na Azam timu za UD Songo ya Msumbiji na Triangle United ya Zimbabwe zimepoteza michezo yao ya hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyopigwa wikiendi hii.

UD Songo iliyozima ndoto ya Simba kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu huu jahazi lao katika Kombe la Shirikisho limeanza kuzama.

Songo ikiwa nyumbani ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Bidvest ya Afrika Kusini, hivyo italazimika kushinda ugenini ili kutinga hatua ya makundi.

Triangle United iliitoa Azam katika hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 2-0, jana Jumapili ilionja joto ya jiwe baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 ugenini kutoka kwa Fc Nouadhibou.

Wakati huohuo; Al Masry iliyoindoa Malindi Fc kwa Jumla ya magoli 7-2, baada ya kuichapa 1-4, Zanzibar na kwenda kumaliza mchezo wenyewe nchini Misri kwa kipigo cha 3-1.

Ikumbukwe kwamba Al Masry iliitoa Simba msimu wa juzi baada ya sare 2-2 nchini Tanzania na kwenda kutoka sare ya 0-0 nchini Misri.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz