Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi wa Simba vs Nkana watajwa

32961 Pic+waamuzi Tanzania Web Photo

Sat, 22 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. AFISA habari wa Shirikisho la Soka  Tanzania  (TFF), Clifford Ndimbo amesema waamuzi wa mechi ya marudiano kati ya Simba SC na Nkana Red Devils, itakaochezwa kesho uwanja wa taifa jijini hapa, wametua salama tayari kwa mchezo huo.

Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo, Ndimbo aliwataja waamuzi hao kuwa wataongozwa na Mkenya Peter Waweru  huku akisaidiwa na Gilbert Cheruiyot,  Tony Kidiya.

“Maandalizi yote yamekamilika kwa kiasi kikubwa na baadae tunategemea kuwa na kikao cha mwisho kabla ya mchezo wenyewe wa kesho, waamuzi wote ni kutoka Kenya na wamefika salama,” alisema Ndimbo.

Baada ya kusema hayo, afisa huyo alizitakia kila la kheri Mtibwa Sugar ambao watatupa karata yao ya pili leo dhidi ya KCCA ya Uganda na Simba ambao wao watacheza kesho na Nkana.

Mtibwa Sugar ambao mchezo wao utachezwa uwanja wa Azam complex, Chamaz  wanahitaji mabao 4-0 ili kusonga mbele kwenye hatua ya mchujo wa mwisho kabla ya kuingia makundi ya kombe la shirikisho Afrika.

Simba wenyewe wanahitaji wa ushindi wa bao 1-0 au wowote wa tofauti ya mabao mawili ili kuingia makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wataondolewa wataingia kwenye mchujo upande wa shirikisho ili kuwania nafasi ya kuingia makundi



Chanzo: mwananchi.co.tz