Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi 17 waula FIFA

Dc703bd6aca03766e037a5788d0e0dcd.jpeg Waamuzi 17 waula FIFA

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waamuzi wa soka Jonesia Rukyaa, Martin Saanya, Emanuel Mwandembwa na Nassoro Mfaume pamoja na wasaidizi Abdulaaziz Ally na Mbaraka Haule wamevuliwa beji za Fifa.

Akizungumza na gazeti hili Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Clifford Ndimbo alisema waamuzi 17 wameteuliwa kuvaa beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2022.

“Waamuzi 17 wamepata beji kwa mwaka 2022 lakini Jonesia jina lake halikurudi kwa sababu hakushiki kozi kutokana na sababu za kifamilia,” alisema Ndimbo. Waamuzi wa kati wapya ni Ahmed Aragija, Nasir Siyah na Tatu Malogo na waliotetea ni Florentina Zablon, Hery Sasii na Ramadhan Kayoko.

Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wapya ni Glory Tesha na Ally Ramadhan na wa zamani waliotetea beji zao ni Soud Lila, Ferdinand Chacha, Frank Komba, Kassim Mpanga, Mohamed Mkono, Hellen Mduma na Janeth Balama. Kwa upande wa waamuzi wa soka la ufukweni ni Jackson Msilombo na Mohamed Ally ambaye amechukua nafasi ya Godfrey Tumaini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live