Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waafrika wampisha mchina kushinda Mbio za Marathon

Beijing Marathon Waafrika wampisha mchina kushinda Mbio za Marathon

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waandaaji wa mbio za nusu marathon za Beijing nchini China wanachunguza tuhuma kuwa wanariadha watatu wa Afrika waliruhusu, kwa makusudi, mwanariadha wa China, He Jie kushinda mbio za Jumapili.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha wanariadha wa Kenya Robert Keter na Willy Mnagat na mwanariadha wa Ethiopia Dejene Hailu wakionesha ishara ya mikono kabla ya kupunguza mwendo na kumpisha He.

He, 25, alimaliza sekunde moja mbele ya wanariadha hao watatu waliomaliza wote kwa pamoja kwa muda sawa katika nafasi ya pili.

Matokeo hayo yalishutumiwa na baadhi ya wananchi wa China kupitia mitandao ya kijamii, imeripoti BBC.

Msemaji wa Idara ya Michezo ya Beijing ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wanachunguza tukio hilo na kuongeza: “Tutatangaza matokeo [ya uchunguzi] mara yatakapopatikana.”

Xstep, kampuni ya michezo ya China iliyodhamini mbio hizo na ambayo ina mkataba na He imeliambia gazeti la China- The Paper- kuwa: “Tukio hili bado linathibitishwa na vyombo kadhaa. Taarifa zaidi zitatolewa haraka iwezekanavyo.”

He, alishinda medali ya dhahabu kwenye michuano ya Asia ya mwaka 2023 mjini Hangzhou na anashikilia rekodi ya nchi hiyo kwenye michuano hiyo.

Wanariadha wote hao hawajasema lolote kuhusu tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live