Moscow, Russia.Ufaransa na Denmark zimefuzu kucheza hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia zikitokea Kundi C baada ya kutoka suluhu.
Ufaransa wamemaliza ikiwa ya kwanza na pointi 7, Denmark ya pili na pointi 5, Peru ya tatu na Australia imepuruza mkia ikiwa pointi.
Katika mechi hizo za mwisho za Kundi C, Australia ilikuwa ilitakiwa kushinda na kuomba Ufaransa iwafunge Denmark ili wafuzu.
Mambo yalikuwa mabaya kwa Australi baada ya kukubalia kipigo cha mabao mawili kutoka kwa Peru.
Peru ilipata bao lake la kwanza dakika 18, lililofungwa na Andre Carrillo kabla ya Guerrero kupachika bao la pili dakika 50.
Hii ni mara ya kwanza kwa Peru kushinda katika mechi Kombe la Dunia tangu ilipofanya hivyo 1982.
Ufaransa sasa watacheza na mshindi kati ya Argentina na Nigeria wakati Denmark atakuwa na kibarua kwa Croatia.