Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#WC2018: Switzerland yaiweka Serbia njiapanda Kombe la Dunia

9808 Swizland+pic TZWeb

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mshambuliaji wa Stoke, Xherdan Shaqiri ameiweka Switzerland katika nafasi nzuri ya kutinga 16 bora baada ya kuifungia bao la usiku dakika ya 89 na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Serbia.

Ushindi huo umeiweka Switzeland katika nafasi nzuri ya kukata tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora m kwenye kundi E linaloongozwa na Brazil yenye pointi 4 huku yenyewe ikifuatia kwenye nafasi ya pili ikiwa na alama 4.

Serbia yenye pointi 3 iliyopo nafasi ya tatu, kutokana na kupoteza mchezo wake wa jana, imejiweka katika mazingira magumu ambapo itatakiwa kushinda mchezo wake wa mwisho huku ikiiiombea Switzerland kupoteza mchezo wake unaofuata.

Costa Rica inaburuza mkia kwenye Kundi E baada ya kupoteza michezo yake miwili jambo ambalo limewafanya kuaga mashindano hayo mapema, huku wakisubiri kukamilisha mchezo wao wa mwisho.

Brazil itakamilisha mchezo wake wa mwisho Juni 27 dhidi ya Serbia,  huku Switzeland watawavaa vibonde Costa Rica.

Michezo hiyo itaamua  kati ya Brazil, Serbia na Switzerland nani ataingia hatua ya 16 bora.

Chanzo: mwananchi.co.tz