Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#WC2018: Salah kustaafu Misri

9942 Pic+salah TZW

Mon, 25 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Grozny, Russia. Nahodha na mshambuliaji mahiri wa Misri, Mohamed Salah, anafikiria kustaafu kuitumikia nchi yake mara tu baada ya nchi hiyo kumaliza mechi za makundi za Kombe la Dunia 2018.

Misri iliyo kundi A, leo itacheza mechi yake ya mwisho hatua ya makundi itakapocheza na Saudi Arabia na baada ya mchezo huo timu hizo zote zitafungasha virago na kureja nyumbani kwa kuwa zimepoteza mechi zote mbili za mwanzo hatua ya makundi.

Kwa mujibu wa mmoja wa marafiki wa karibu wa Salah, mshambuliaji huyo wa Liverpool, angali na lindi la mawazo akijiuliza iwapo arejee Misri na wachezaji wenzake ama atokomee zake Uingereza.

Sababu za Salah kufikia hatua hiyo imeelezwa kuwa ni mambo ya kisiasa ikielezwa watawala wa Misri wamekerwa na ukaribu wake na kiongozi wa Chechnya, Ramzan Kadyrov, ambaye tayari amempa mshambuliaji huyo uraia wa heshima wa Chechnya.

"Mohamed Salah ameumizwa na namna anavyoanza kuhusishwa na masuala ya kisiasa nchini Misri, hivi sasa anafikiria kustaafu kuitumikia timu ya Taifa lake na pengine akaamua kutorejea kabisa Misri.

Hofu yake inatokana na namna walivyotendewa wachezaji wengi wa zamani waliodhaniwa kutoiunga mkono serikali ya nchi hiyo akiwemo nahodha msaidizi wa zamani wa nchi Mohamed Aboutrika na wengine kadhaa ambao mali zao zote zimetaifishwa na wao kusoteshwa mahabusu.

Chanzo: mwananchi.co.tz