Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#WC2018: Dua zote za Afrika kwa Senegal leo

10228 Senegal+pic%255C TZW

Thu, 28 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moscow, Russia. Wawakilishi pekee wa Afrika waliosalia kwenye kinyang’anyiro cha Fainali za Kombe la Dunia, Senegal inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kuona kama itawapa furaha.

Senegal itashuka dimbani leo kukabiliana na Colombia katika mchezo wa mwisho wa kundi H, ingawa hata sare itawawezesha kutinga hatua ya 16 bora, lakini Senagal iliyoruhusu bao la dakika za mwisho ilipocheza na Japan, leo inapaswa kuwa makini katika dakika za lala salama.

Hata hivyo mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Samara Arena, mjini Samara hautakua rahisi kwao kwa sababu, Colombia yenye pointi tatu itapambana kusaka ushindi ili nayo itinge hatua ya 16 bora.

Senegal inabeba matumaini ya Waafrika kutokana na Misri, Morocco, Tunisia na Nigeria, kung’olewa katika hatua ya kwanza ya Fainali hizo zinazoendelea katika miji kadhaa ya Russia.

Katika kundi H, Senegal na Japan zinachuana kileleni baada ya kila timu kuwa na pointi nne huku Colombia ikiwa ni pointi tatu na Poland haina pointi na haitegemewi kuizuia Japan, zitapokwaana kwenye uwanja wa Volgograd Arena, Volgograd.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz