Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viungo wambeba Zahera Yanga SC

10775 PIC+VIUNGO TanzaniaWeb

Wed, 8 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera anaendelea na maandalizi ya timu yake kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku akiwataja wachezaji wa viungo watakuwa mhimili wake katika mashindano hayo msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili jana, Zahera alisema endapo kiungo mpya Mohammed Issa ‘Banka’ atajiunga haraka katika kikosi chake atakuwa na fursa nzuri ya kutengeneza timu imara.

Banka ambaye amesajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar, hajajiunga na timu hiyo baada ya kuomba ruhusa maalumu akiungana na mshambuliaji Ibrahim Ajibu na kipa kinda Ramadhani Kabwili.

Zahera alisema timu yake imelamba dume kumsajiki kiungo Feisal Salum ‘Totoo’ ana mpango wake ni kumchezesha pacha na Mkongomani Pappy Tshishimbi.

Kocha huyo alisema Feisal ameonyesha ukomavu mkubwa na akifanikiwa kuwaunganisha vyema Banka ataimarisha eneo la kiungo na kusukuma mashambulizi.

Katika mazoezi ya timu hiyo Feisal aliyesajiliwa akitokea JKU ya Zanzibar amekuwa akionyesha kiwango kikubwa cha kupiga pasi zinazofika vyema sanjari na kurudi chini haraka kusaidia ukabaji na kumfanya Zahera kila wakati kumsifu.

Aidha, kocha huyo alisema kama atafaulu kuwapanga pamoja anaweza kumtumia kiungo Deus Kaseke kutokea pembeni kushoto huku Mrisho Ngassa akitokea kulia.

Wakati Zahera akijipanga hivyo bado atajikuta katika wakati mgumu katika kuchagua viungo kufuatia kundi zaidi la viungo kama Jafari Mohammed, Thabani Kamusoko nao wakionekana tayari kuchukua nafasi katika kikosi hicho.

“Namuhitaji sana Banka kuna kitu nataka kufanya hapa lakini akichelewa hivi naumia kichwa ni kiungo mzuri nilimuona ndiyo maana nikasema asajiliwe,”alisema Zahera.

“Tumepata viungo wazuri ambao wanajua kufanya majukumu yao tunaweza kuwatumia viungo watatu mpaka wanne kwa mara moja na kama tukiwaunganisha tunavyotaka tunaweza kuwa na timu imara zaidi.

“Angalia kipaji cha Feisal ni kijana mdogo lakini kazi yake uwanjani ni kubwa sasa huyu kama akicheza sambamba na Pappy ukiongeza na Banka tutakuwa imara kupambana na yoyote.

“Huku pembeni tunaweza kuwatumia Kaseke na Ngassa wanajielewa vizuri...ninavyoona timu yetu ni imara na kama tungepata muda huu wa mazoezi kabla ya mechi zile mbili dhidi ya Gor Mahia tukiwa na hawa wachezaji wote nafikiri tusingepoteza kabisa.”

Chanzo: mwananchi.co.tz