Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana wacheza Sarakasi wa Bongo Tanzania watikisa Australia’s Got Talent

AGT2022 Ramadhani Brothers 06 Resize  Scaled E1663619289900 Vijana wacheza Sarakasi wa Bongo Tanzania watikisa Australia’s Got Talent

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasanii wawili wa sarakasi kutoka Tanzania Ibrahim na Fadhili Ramdhan wanaounda kundi la The Ramadhan Brothers wamefanikiwa kuibuka Washindi wa hatua ya kwanza kwenye shindano la Australia’s Got Talent mwaka 2022 na sasa wataendelea kwenye hatua inayofuata ya Shindano hilo.

Hii ni mara ya kwanza kwao kufika Australia na mara ya kwanza kwao kufanya onesho la sarakasi kwenye show kubwa ya TV ambapo ubunifu wao uliibuka kivutio kikubwa kwa Watazamaji na Majaji akiwemo Jaji mmoja ambaye alikiri kuifahamu Tanzania na kusema amewahi kufika Mlima Kilimanjaro.

Imeelezwa kuwa zawadi ya shindano hilo ni USD 100,000 (Tsh. Milioni 230) ambazo wamesema wakizipata watazitumia kuwainua Vijana wenzao wa Afrika wenye ndoto za kufikia mafanikio na kuna Shule ya vipaji ambayo wataisaidia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live