Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo wataja dawa kuboronga waamuzi

16115 Pic+waamuzi TanzaniaWeb

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati sakata la waamuzi kuboronga katika mashindano likionekana kikwazo katika maendeleo ya soka nchini, wadau wametaja suluhisho la kupata marefa bora watakaonusuru mchezo wa soka nchini.

Kwa muda mrefu waamuzi wa soka wameonekana kuwa kikwazo cha maendeleo ya mchezo huo, baada ya kukumbwa na kashfa mbalimbali ikiwemo kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za soka na matukio ya rushwa.

Hivi karibuni, Bodi ya Ligi iliwafungia waamuzi wanne, Jimmy Fanuel, Nicholas Makaranga, Jamada Ahmada na Athumani Lazi kila mmoja miezi mitatu kwa kuvunja kanuni ya 39(i) ya udhibiti wa waamuzi.

Wakati Fanuel akishindwa kutafsiri sheria kwenye mchezo wa Azam dhidi ya Mbeya City, Jamada aliboronga katika mechi baina ya Singida United na Mwadui FC, Makaranga akivurunda Ruvu Shooting dhidi ya KMC sanjari na Lazi.

Akizungumzia chanzo cha waamuzi hasa wa Ligi Kuu kufungiwa mara kwa mara, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania (TFF), Salum Chama alisema kukosekana kwa mafunzo na mazoezi ya utimamu wa mwili kumechangia waamuzi kufanya vibaya.

Chama alisema wameanza mkakati wa kuandaa mafunzo mikoani kwa waamuzi ili kuwajengea uwezo wa kutafsiri vyema sheria 17 za soka.

Kauli ya Chama imewaibua wadau wa soka akiwemo mwamuzi nguli wa zamani nchini Omar Abdulkadir na Othumani Kazi.

Kazi alisema waamuzi nchini wanatakiwa kutengezewa mazingir bora ya kufanya kazi siyo kumfungia.

“Ninadhani tunapaswa kuiga nchi za wenzetu ambapo mwamuzi akikosa anashushwa daraja anachezesha madaraja ya chini ili kwenda kujifunza zaidi,” alisema Kazi.

Abdulkadir alisema waamuzi wana wajibu wa kutambua wana dhamana na soka la Tanzania, hivyo wanapaswa kusimamia vyema sheria 17 kwa maendeleo ya soka nchini.

“Mwamuzi ukiharibu lazima ujue unaharibu mpira wa Tanzania. Lazima wachezeshe kwa haki kwa sababu teknolojia ya sasa ni pana na inaweza kubaini madudu yanayofanywa na waamuzi,” alisema Abdulkadir.

“Wenzetu mwamuzi akikosea anapewa mechi nyingine na nyingine ili ajirekebishe sio kumfungia,” alisema Katibu Mkuu wa Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT), Oden Mbaga.

Chanzo: mwananchi.co.tz