Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo wapya Yanga waonya

49689 VIGOGO+PIC

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

HUKO Yanga mtapapenda wenyewe tu, ile Kamati iliyoundwa juzi ya usimamizi wa timu jamaa hawataki kuremba na tayari wameanza vikao vizito wakipeana majukumu.

Lakini, kwa kauli iliyotolewa na Mwenyekiti na Makamu wake shughuli mbona itakuwepo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Lucas Mashauri ameliambia Mwanaspoti, mara baada ya kutangazwa walianza mipango kabambe kuhakikisha Yanga inakuwa moto.

Achana na matokeo ya jana kule Mwanza kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Alliance, Yanga inayokuja itakuwa balaa kwelikweli.

Mashauri, ambaye usajili wa beki Kelvin Yondani na kiungo Feisal Salum ulifanyika ndani ya moja ya ofisi zake, alisema mara baada ya kumaliza mchezo na Alliance watakutana tena kupanga mikakati ya mechi moja kwenda nyingine.

Bosi huyo alisema hakuna kinachoshindikana kwa aina ya kamati iliyoundwa na imewakutanisha watu wenye kiu ya kuiona Yanga inafanikiwa.

“Unatuona sasa tunatoka katika vikao haya ni majukumu na tumeanza kutekeleza, hatuna muda wa kupoteza na tangu juzi ni vikao vya mipango ya kazi,” alisema Mashauri akiwa anatoka katika hoteli moja kubwa katikati ya jiji akiwa na makamu wake Said Ntimizi.

Ntimizi huyu hapa

Naye Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ntimizi alisema kama Yanga itakuwa moja kwa kila mwanachama kuipa ushirikiano kamati yao hakuna atakayeisumbua na watamchapa yoyote katika mechi zao.

Ntimizi alisema klabu nyingi pinzani kwao hazitaki kuona Yanga inatulia na ni nafasi kwa Wanayanga sasa kutulia na kuepuka mgawanyiko.

“Sidhani kama klabu yetu kutakuwa na umoja kama kuna mtu anaweza kutoka salama kwa Yanga sote tunatakiwa kuungana ili tufanikiwe,” alisema Ntimizi.

“Kamati yetu ina ari kubwa ya kupata mafanikio, lakini kama kutakuwa na kupingana ndani ya klabu tukipeana ushirikiano kila kitu kitakuwa chepesi.



Chanzo: mwananchi.co.tz