Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vestappen afikiria kumalizana na F1

Max Verstappen B Max Verstappen

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Miaka 26 tu aliyonayo kwa sasa dereva bingwa wa mbio za magari ya langalanga duniani (formula one) Max Verstappen, ameanza kujitabiria kuachana mapema na mbio hizo ghali zaidi duniani.

Verstappen ambaye alitia fora kwenye mbio za mwaka jana 2023, kwa kushinda 19 kati ya 22 za msimu mzima, ameeleza hana mpango wa kukaa kwa muda mrefu kwenye mbio hizo kama magwiji wengine waliopita.

Verstappen anayetumia Kampuni ya Red Bull, anatajwa kujiandaa kuachana na mbio hizo mapema japo hajaweka wazi mwaka gani ataachana nazo, lakini kutoa kauli hiyo akiwa na miaka 26 inawezekana asiendelee kushindana kwenye mbio hizo baada ya kufikisha miaka 30.

Mbali na hilo, haijafahamika kama bingwa huyo mara tatu wa mbio hizo za magari anatarajia kuacha akiwa ameshinda mataji mangapi kwani rekodi ya jumla ni mataji saba inayoshikiliwa na Michael Schumacher na mpinzani wake wa sasa, Lewis Hamilton kwa pamoja wakiwa na mataji saba, ikiwa ni manne zaidi ya aliyonayo Verstappen kwa sasa.

Chanzo: Mwanaspoti