Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Zahera ambeba Urikhob

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amemkingia kifua mshambuliaji Sadney Urikhob kuwa ni mchezaji atakayekuwa msaada mkubwa kwa klabu yake na kuomba wampe muda ili kudhihirisha hilo.

Zahera aliyasema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Kariobang kwa kutoka sare ya bao 1-1 na kuongeza kuwa kwa muda mchache alioutumia kukaa kambini na wenzake haujatosha kumuweka fiti na kuzoea hari soka la Tanzania.

Alikiri kuwa mchezaji huyo pamoja na kuonyesha kashikashi uwanjani alikuwa ni mzito wa kufanya maamuzi ambayo yangeweza kusaidia timu kufanya vizuri kwa kupata matokeo ya mapema zaidi.

"Aliingia kambini wakati wenzake tayari wameshaanza mazoezi anamuda mfupi wa kujiandaa pamoja na wenzake naweza kusema akiwa fiti ndiye atakayekuja kuwa mshambuliaji atakayeibeba timu yetu katika mashindano mbalimbali," alisema na kuongeza kuwa.

"Kikosi cha Yanga kimebadilika kwa kiasi kikubwa na niliongea na wachezaji kuwa waingie uwanjani kucheza mpira washinde au wasishinde hakuna kitakachoangaliwa zaidi ya kuonyesha uimara wao uko wapi na mimi nimeona tuna kikosi kizuri sana," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz