Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Zahera: Yondani, Kakolanya wanadai mishahara

Wed, 21 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema sababu ya nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani na kipa Benno Kakolanya kujiengua katika safari ya Kanda ya Ziwa ni madai yao ya mishahara ya miezi tano.

Yondani na Kakolanya wameshindwa kujiunga na timu hiyo iliyoondoka jana asubuhi kwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Mwadui na Kagera Sugar.

Akizungumza kuhusu sababu za wachezaji hao kujiengua katika kikosi hicho kocha Zahera alisema wachezaji hao wanamadai ya mishahara ya miezi mitano.

“Nimefika hapa Mwanza, lakini wachezaji Yondani na Benno hawapo hapa kwa sababu ya madai yao.”

Zahera alisema anajua watu wengi wanataka kujua ni mchezaji gani tunataka kumsajili, lakini kwanza tunatakiwa kuboresha mikataba ya hawa waliokuwepo hapa.

“Kumpata mchezaji mpya kwa sasa inatakiwa fedha nyingi, itakuwa vigumu kumnunua mchezaji halafu baadaye ukamkopa.”

Kocha Zahera ameandika ujumbe wake kwa Kiswahili cha tabu kilichochanganyika na kikongo kuhusu sakata hilo:

Salama vituyote ni vizuri kuanguvu ya munyezi mungu.team ili fika vizuri apa shinyanga.na mimi nalikuta team apa shinanga .ila wamenipasha kama watchezaji wa wili wamekataha kusafiri sababu ya mwezi tano ya mishahara yaho awapewe .kevin yondani .na BENO gool keeper

Nazani nyinyi wote munangoja kuniuliza abari kocha dirisha kidogo imefunguliwa ni je? Ku ngambo ya yanga? Ile nyinyi wite munangoja niwape abari. Aya mimi nasema kua kupata mchezaji mupia inaomba transfert.inaomba kusikilizana mshahara.kusikilizana modaliti ya contrat na ile yote kuasikuyaleo sione hata namna moja yakuweza kusumulia na wachezaji wowote sababu atueneze ile ma conditions na waeleza.uta anzia wapi ? Na utamalizia wapi masungumzo na watchezaji wa mpia ? Viongozi wengine wameniambia nitafute watchezaji.sasa limi nitafute muchezaji nisumulie naye nini? Wakati team aieneze ma conditions.ya transfert .ya vitu yote inaomba kua kununua mchezaji wamupia.ni ivio naona kama leo iyi tunaendeleya nawale wale wachezaji. sababu mbele ya kukopesha wachezaji wa yanga ku team ingine inafaha kuanza kujuwa nani ata komboa.



Chanzo: mwananchi.co.tz