Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Zahera,Tshishimbi wawaita mashabiki Taifa kesho

Sun, 4 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameungana na nahodha wale Papy Tshishimbi kuwataka mashabiki wa kujaa kwa wingi uwanjani kesho Jumapili.

Yanga leo Jumamosi mchana imefanya mazoezi yake ya kwanza na mwisho Uwanja wa Uhuru kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya ambao ni mabingwa wa Kombe la Sportpesa.

Zahera amesema kazi ya kuandaa timu ipo hatua nzuri na sasa wako tayari kuwaonyesha wanachama na mashabiki wao ubora walionao.

Zahera amesema hatagemei kuona shabiki wa Yanga anayeipenda timu hiyo kukaa nyumbani bila kwenda uwanjani.

Kocha huyo amesema kesho ni siku muhimu kwa Wanayanga kuwaonyesha mapenzi yao wachezaji wao wapya ambao wamesajiliwa kwa fedha zao.

Naye kiungo na nahodha wa timu hiyo Tshishimbi amesema baada ya kambi na mazoezi ya mkoani Morogoro sasa wako tayari kutoa burudani.

Tshishimbi amesema kila mchezaji amejiandaa vyema kupitia kambi yao na kwamba watafurahi kuona mashabiki wao wameujaza uwanja wa Taifa.

Chanzo: mwananchi.co.tz