Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Yanga yapiga kambi hoteli ya ushindi

14339 Pic+yanga TanzaniaWeb

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigali, Rwanda. Yanga imetua salama jijini Kigali, Rwanda lakini hoteli waliyofikia ina rekodi nzuri kwao kwa kupata ushindi mkubwa dhidi ya timu za hapa.

Yanga imefikia katika jiji la Kigali na kuweka kambi katika hoteli ya Mirror iliyopo umbali mfupi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali.

Awali kabla ya kufikia hapo Yanga iikuwa haijulikani itafikia hoteli gani ambapo mabosi wa Chama cha soka nchini Rwanda (Ferwafa) walionekana kuchukizwa na ukimya wa timu hiyo wasijue wanafika lini.

Mara baada ya kuwasili Yanga ilijiandalia usafiri yenyewe na kufikia hoteli ya Mirror ambayo waliitumia misimu miwili iliyopita.

Hoteli hiyo Yanga waliwahi kuitumia wakati wakitua hapa kuumana na APR katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Amahoro Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao 3-1 kisha timu kurudiana jijini Dar es Salaam na kutoa sare ya bao 1-1 na kuivusha Yanga.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omari Kaya alisema haakuwa na presha katika kufika kwao hapa kwa kuwa tayari walishafanya mawasiliano na hoteli mbili tofauti.

Kaya alisema wameamua kufikia hoteli ya hiyo kufuatia makocha kuridhika nayo kutokana na utulivu uliopo katika eneo hilo.

"Tumeona wenyeji wetu wanalalamika lakini tulikuwa tunajua tunachokifanya,tulishafanya maandalizi yetu karibu katika kila kitu,"alisema Kaya.

"Tumeona tufikie pale Mirror hata makocha wamekubaliana na mazingira ya pale wameona timu haitakuwa na usumbufu."

Chanzo: mwananchi.co.tz