Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Yanga kumuaga JPM leo Uhuru

Video Archive
Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

UONGOZI wa klabu ya Yanga pamoja na kikosi chao leo Jumapili asubuhi watakuwa miongonj mwa wananchi watakaokuwa  katika msafara wa kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Yanga jana Jumamosi jioni ilisimamisha kambi yao na kutoa fursa kwa wachezaji wao leo Jumapili kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais huyo aliyeaga Dunia Machi 17 jioni baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.

Wachezaji na viongozi wa klabu hiyo watakutana makao makuu ya klabu saa 3:00 asubuhi kisha ndio msafara wao utaanza kwenda katika uwanja wa Uhuru.

Kupitia katika ukurasa wao rasmi wa Instagram ulielezea kuwepo kwa tukio hilo kwa wachezaji na viongozi wao siku ya leo.

Shughuli za kuaga mwili wa marehemu Magufuli zilianza jana kwa kuongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mawaziri, viongozi na kufuatiwa na wananchi wa kawaida.

Rais huyo amefariki huku akikumbukwa kwa uwezo wake  wa kusimamia kile ambacho ana kiamini mpaka kitimie kama alivyokuwa anataka.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz