Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wachezaji wa Simba walivyosherehekea siku ya kuzaliwa ya Tshabalala

Sat, 2 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

NAHODHA Msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala', amekipata cha moto kwenye mazoezi ya leo Ijumaa asubuhi. Simba imefanya mazoezi viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na mara baada ya kumalizika Tshabalala alipasuliwa mayai. Novemba Mosi, ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Tshabalala na baada ya mazoezi kumalizika wachezaji wenzake walimpasulia mayai ya kuku mwili mzima. Wachezaji wa Simba walimkimbilia Tshabalala na kumshika huku wengine wakimuweka katika dumu la maji na kuanza kumlowesha mwili mzima. Baada ya kutoka hapo kuna wachezaji waliompasulia mayai hayo huku wengine walimbeba na kumpeleka pembeni ya uwanja na kumweka kwenye matope ambapo pia alimwagiwa maji machafu. Tshabalala alipata nafasi ya kuwachomoka na kukimbia akiwaacha wenzake waliokuwa wamemmwagia maji, kumpaka matope na kumpasulia mayai.

Chanzo: mwananchi.co.tz