Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Taifa Stars yavunja kambi, CAF yaahirisha CHAN 2020

Video Archive
Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuvunja kambi ya timu ya Taifa Tanzania iliyokuwa ikijiandaa na mashindano ya CHAN muda mfupi baada ya CAF kusitisha michuano hiyo kwa muda usiojulikana.

Mapema leo mchana Waziri Mkuu Tanzania, Kassim Majaliwa alitangaza kusimamisha michezo yote nchini pamoja na kufunga shule za awali mpaka kidato cha sita kwa siku 30.

Akizungumza baada ya mazoezi ya jioni kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amethibitisha kuvunjwa kwa kambi hiyo hadi pale hali itakapokuwa shwari.

"Hakuna jinsi inabidi tujihahadhari na ugonjwa huu kwa sababu serikali imeshasema na ugonjwa huu ni hatari," alisema Ndayiragije.

"Tukitoka hapa tunarudi kambini na kila mchezaji ataondoka kuelekea nyumbani kwake," alisema Mrundi huyo.

Wakati Stars ikivunja kambi hiyo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imetangaza kuahirishwa kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN2020) hadi itakapotangazwa tena pamoja wenyeji Cameroon kuwa tayari kwa fainali hizo za mwezi ujao.

Pia Soma

Advertisement
CAF imechukua uamuzi huo leo Jumanne kutokana na tishio la ugonjwa wa Corona ambao tayari umechukua maisha ya watu zaidi ya 5000 dunia nzima.

Mashindano hayo yalitakiwa kuanza kutimua vumbi Aprili 4-25, 2020 na wenyeji Cameroon walisema wapo tayari kwa mashindano hayo wakiwa wamejipanga kuhakikisha wachezaji, viongozi na mashabiki wote wanakuwa salama katika kipindi chote cha mashindano.

Lakini kamati ya CAF iliyotembelea Cameroon imeiomba kamati ya afya kuchukua uamuzi wa kusimamisha mashindano hayo kwa sababu ya kusambaa kwa virusi vya corona.

"Pamoja na hali kuonekana kuwa salama ndani ya Cameroon, lakini kwa ushauri wa WHO, hali ya ugonjwa huo bado si salama na vigumu kujua nini kitatokea katika siku chache zijazo;

"Usafiri ndani barani Afrika umekuwa mgumu kwa sababu mataifa mengi yamefunga mipaka yao, pamoja na kuwepo kwa mazuio ya watu kuingia nchi moja na nyingine, kutokana na makatazo ya serikali mbalimbali;

"Kwa sababu hizo hatuna sababu ya kuhatarisha maisha ya watu, tumechukua uamuzi wa kamati ya Afya kuahirisha mashindano ya CHAN." Ilisema barua ya CAF kwenda kwa wanachama wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz