Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: SportPesa yaileta Sevilla kucheza Yanga au Simba

Video Archive
Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Dar es Salaam. Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa kwa kushirikiana na La Liga imetangaza kuileta klabu ya Sevilla nchini Tanzania kwa ajili ya ziara ya kimichezo inayokwenda kwa jina la “SportPesa Laliga Challenge".

SportPesa ambao ni washirika rasmi wa michezo ya kubashiri Afrika wa Ligi hiyo maarufu duniani ya La Liga, wanatazamia kuwaleta nchini Mabingwa hao mara tano wa michuano ya UEFA Europa ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya msimu mpya wa 2019/2020.

Wakiwa nchini Tanzania, Sevilla ambao pia ni mabingwa mara moja wa La Liga, watacheza na moja ya timu washirika wa SportPesa kati ya Simba au Yanga kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Msisimko wa Kimataifa

Akizungumzia ugeni huo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Ndugu Tarimba Abbas amesema ziara hiyo ya Sevilla nchini ni muendelezo wa utekelezaji wa sera ya kampuni ya kuendeleza michezo nchini.

“SportPesa tunaendesha biashara yetu kwa kujihusisha na maendeleo ya soka kwenye nchi tunazoendesha shughuli zetu kwa kushirikiana na wadau husika huku tukitumia washirika wetu wa kimataifa kuleta maendeleo hayo.

“Mara ya mwisho dunia ilishuhudia klabu ya Everton ikitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza na muitikio ulikuwa ni wa kipekee.

“Kutokana na SportPesa kuwa na ushirika na taasisi kubwa za soka duniani kama La Liga, tukaona basi ni vyema kuendeleza msisimko wa kimataifa kwa kuileta klabu ya Sevilla nchini Tanzania ambayo inacheza kwenye Ligi hiyo bora duniani.

“Lengo ni kuionesha dunia kuwa Tanzania ni mahala sahihi kwa vilabu vikubwa duniani kuja kwa ajili ya ziara za maandalizi ya Ligi bila kusahau kuvinadi vipaji adhimu vya soka vilivyosheheni”.

 

Nafasi ya kujifunza

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Kidao Wilfred amesema ujio huo wa Sevilla ni fursa pekee kwa wachezaji wetu na wadau wa sekta ya mpira nchini kujifunza.

“Tunashukuru kupata ujio wa timu kubwa kama Sevilla ambayo inacheza kwenye Ligi kubwa duniani ya LaLiga.

“Unapopata nafasi ya timu yako ya nchi kucheza na timu kubwa kama hiyo ni jambo na la heshima na lina faida nyingi kwa maana ya kujitangaza kwasababu dunia nzima itajua kwamba Sevilla ipo Dar es Salaam, lakini pia wachezaji wetu watapata nafasi ya kujifunzakutoka kwa wenzao sambamba na kuonekana na kumulikwa na wataam wa kusaka vipaji duniani.

“Si hivyo tu, lakini pia makocha, madaktari na viongozi wa juu wa vilabu watapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao jinsi wanavyoendesha mambo yao kwa weredi.

“Maandalizi kwa ajili ya mtanange huo yanaendelea vizuri na sisi kama Shirikisho la soka nchini tutahakikisha kuwa tunaiandaa mechi hiyo kwa kiwango cha kimataifa kwa kushirikiana na washirika wetu, kampuni ya SportPesa na tutahakikisha tunawaunga mkonokwenye jitihada zao za kuendeleza michezo nchini ,” alihitimisha Ndugu Wilfred.

 

Wakiwa nchini Tanzania, wachezaji pamoja na viongozi wa Sevilla watashiriki katika semina mbalimbali za uwezeshaji kwa viongozi wa soka nchini, kliniki za soka, shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na utalii kabla ya kucheza dhidi ya Simba au Yanga.

 

Hii itakuwa ni ziara ya pili kubwa ya kimichezo nchini kuandaliwa na kampuni ya SportPesa Tanzania ikihusisha timu kutoka moja ya Ligi kubwa barani Ulaya.

 

Julai 2017, SportPesa waliileta klabu ya Everton nchini ambapo dunia ilimshuhudia Wayne Rooney akiichezea Everton mechi yake ya kwanza tangu mwaka 2004 katika ardhi ya Tanzania akiwa ametoka kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Manchester United.

 

Kuhusu SportPesa

SportPesa ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha na michezo na habari za burudani. Kupitia majukwaa yetu tunatoa matokeo ya mechi papo hapo na kwa nchi nyingine tunatoa huduma ya michezo ya kubashiri na ushindi kwa wateja wetu.

 

Sisi ni kampuni tuliyojidhatiti kutoa huduma na kuwekeza katika maendeleo ya michezo na jamii zetu. Tunatumia nguvu ya michezo kuunganisha watu kokote ulimwenguni; kuwapa wateja wetu msisimko halisi wa michezo, kuviongezea vilabu kipato na kutoa fursa kwa wanajamii.



Chanzo: mwananchi.co.tz