Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Shabiki Simba aliyetembea kwa mguu afichua mazito

Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

SHABIKI wa Simba aliyetembea kwa mguu kutoka Mbeya mpaka Dar es Salaam, Ramadhan Salum Mohamed amefichua kitu kikubwa ambacho hatakisahau katika safari yake ni kashi kashi dhidi ya askari.

 Anasimulia kwamba alipofika Chalinze alifika moja kwa moja mpaka kituo cha polisi, badaye alipotaka kuendeleana safari mashabiki wa Simba walimzunguka wakimshangaa.

 Kitendo hicho kilimkera askari ambaye alidhani anafanya maandamano akaanza kumvuta na mashabiki pia wakimvuta.

 "Nilikuwa nimechoka sana, nilihisi kufa, mashabiki wananivuta askari ananivuta, nikabaki kutazama niangalie mwisho wangu, badaye nikarudi kituoni askari waliokuwepo wakanitetea. "Nimetumia siku 10 kutembea tangu 26 Machi mpaka Aprili 24, kikubwa ilikuwa nikuja Dar kwa mguu kurudi ningedandia hata lori.

 "Mikumi niliombewa lifti na maskari ili kunivusha eneo la wanyama kwani kila hatua nilikuwa nafuata sheria za nchini, "anasema. Anasema anamuomba Mungu Simba ishinde dhidi ya TP Mazembe ili kumtia moyo kwa kile alichokifanya kwa kutembea kwa mguu baada ya hapo ana mpango wa kupanda mlima Kilimanjaro.

"Dhamira yangu imetimia naipenda Simba hii nimerithi kutoka kwa baba yangu mzazi,wachezaji wajitume waelewe kwamba tunahitaji kuona wanafanya kazi yakufurahisha mashabiki"anasema.

 

APOKEWA KISHUJAA KARIAKOO

Alipofika mitaa ya Msimbazi ambako ndio makao makuu ya klabu ya Simba, alipokewa kishujaa na mashabiki wenzake ambao wamemuahidi kumrudisha kwa ndege

 



Chanzo: mwananchi.co.tz