Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Rais TFF amlilia Rajab Kessy

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema amepokea kwa mshtuko na majonzi kifo cha aliyekuwa mtunza vifaa msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ marehemu Kessy Rajab.

Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Kessy akiwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu wakati maandalizi ya kuuhifadhi mwili wake yakiendelea.

Taaarifa hiyo ya TFF ilieleza kwamba, msiba utakuwa nyumbani kwake Kurasini jijini Dar es Salaam akaribu na ofisi za Uhamiaji wakati taratibu zingine za maziko zitatolewa hapo baadaye.

Taarifa za kufariki dunia kwa Kessy, zilianza kusambaa jana jioni wakati mechi ya Simba ikiendelea dhidi ya Nkana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Awali, ilielezwa kwamba baada ya kutokea sintofahamu uwanjani hapo, Kessy aliwahishwa hospitalini na gari ya wagonjwa iliyokuwapo ndani ya Uwanja wa Taifa.



Chanzo: mwananchi.co.tz