Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mgosi: Kagere ana kizizi cha Simba

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Staa wa zamani wa Simba, amesema kama Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi wakitulia na kufanya umakini katika safu yao basi Yanga watapigwa 7-0.

Mgosi anasema hakuna cha ushirikina bali anazungumzia kiufundi namna ambavyo Simba wapo vizuri kwa mchezaji mmoja mmoja akidai tofauti na Yanga.

Anasema mara nyingi kinachowaangusha Simba ni wachezaji kuvimba vichwa wakisahau Yanga watakuwa wanahitaji heshima mtaani.

"Simba kiufundi ipo vizuri ukilinganisha na Yanga kwa mechi zao tatu za mwisho lakini kwa kuwa ni watani basi lazima Kagere, Okwi na Bocco wafanye kweli.

"Jambo lingine ambalo ni tatizo kwa Simba na Yanga ni viwango vya wachezani unavyomuona leo sivyo anavyokuwa kesho sio watu wa kulinda uwezo wao.

"Lakini pia lazima mwanafamilia wa soka ajue wazi kwamba kuna matokeo ya aina tatu kufungwa, ushindi na sare kwani pande zote mbili zinataka kucheka"anasema Mgosi.



Chanzo: mwananchi.co.tz