Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO : Lukumay, Nyika wajiuzuru kupisha uchaguzi Yanga

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kaimu mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Hussein Nyika wametangaza kujiuzuru nafasi zao ili kupisha mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo.

Uamuzi wa Lukumay na Nyika umekuwa wiki chache baada ya mwenyekiti wa baraza la wadhamini la Yanga, George Mkuchika kugusia kuwa wamekubaliana klabu hiyo itafanya uchaguzi kamili na sio wa kujaza nafasi na kwamba wajumbe waliobaki watajiuzulu kupisha uchaguzi huo.

Wakizungumza katika mkutano na wanahabari katika ofisi za makao makuu ya Yanga mtaa wa Jangwani na Twiga, Lukumay amesema uamuzi wao huo akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Hussein Nyika ni kupisha uchaguzi kamili wa klabu hiyo.

 

Lukumay ambaye alichaguliwa na wanachama amesema wameamua kuchukua uamuzi huo katika kusuka uongozi kamili wa klabu yao kwa uchaguzi kufanyika kuanzia nafasi ya mwenyekiti mpaka wajumbe nane wa kamati ya utendaji.

Amesema pia wamelazimika kuchukua uamuzi huo kutokana na mpaka wiki mbili zilizopita walibaki wajumbe wanne wa kuchaguliwa, lakini baadaye wengine wawili walijiuzulu na kubaki wao wawili.

Aidha Lukumay mbali na kuwashukuru wanachama amesema klabu yao bado iko salama kutokana na sasa itakuwa chini ya Baraza la Wadhamini ambao watatoa muongozo mpya ndani ya siku chache.

Naye Nyika ameungana na Lukumay katika uamuzi huo pamoja na sababu hizo akisema kujiuzulu kwake hakujamfutia uanachama wake na kwamba wataendelea kuwa mwanachama mtiifu pia akiwa tayari kushirikiana na viongozi wapya watakaopatikana endapo wataona anafaa kufanya hivyo

 



Chanzo: mwananchi.co.tz