Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Kocha Simba awashtua Taifa Stars kwa Burundi

Video Archive
Tue, 3 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kesho Jumatano itashuka uwanjani kucheza mechi yake ya kwanza ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Burundi, lakini kocha wa zamani wa Simba, Masoud Djuma ameibuka na kusema mechi ngumu kwani wachezaji wa timu hizo wanafahamiana.

Djuma aliyewai kuifundisha Simba alisema mbali na wachezaji kufahamiana, lakini ujirani wa nchi hizo pia utachangia kuongeza ugumu wa mechi hiyo.

"Tanzania nimekaa zaidi ya mwaka kuna wachezaji wazuri ambao niliwaona na ambao wapo timu ya Taifa, lakini hata Burundi nao wana wachezaji wazuri wazawa na wale ambao wanaocheza nje,"

"Burundi wanaweza kucheza vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa maana hiyo Stars, wanatakiwa kuwa makini zaidi kama ambavyo Stars watakapocheza mechi ya marudiano Uwanja wa Taifa wanabadilika na kuwa wakali.

"Timu ambayo itakuwa na maandalizi mazuri na wachezaji kujitolea dakika zote 90 ndio itaondoka na pointi tatu, lakini watakaofanya makosa mengi hasa safu ya ulinzi kulingana na washambuliaji wazuri itapoteza mchezo," alisema Djuma

Stars baada ya kucheza mchezo wa kwanza na Burundi, ugenini watarudiana Septemba 8, katika mechi itakayochezwa uwanja wa Taifa na mshindi wa jumla ndio atasonga hatua inayofuata.

Pia Soma

Advertisement   ?

Kikosi cha Stars kimeondoka leo Jumanne asubuhi kuelekea Bunjumbura, Burundi, msafara wa wachezaji 21.

Chanzo: mwananchi.co.tz