Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Kampuni ya Romario kuijaza mapesa Simba

Video Archive
Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Klabu ya Simba imetia saini mkataba wa miaka miwili na Kampuni ya Romario kwa ajili kuwapa vifaa vya mazoezi.

Vifaa ambavyo Simba ifaidika navyo katika mkataba huo ni jezi, vizibao na mipira.

Akizungumza leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Crescentius Magori alisema mkataba huo utakuwa na thamani ya Sh600 milioni na kila mwaka watapata Sh300 milioni.

Magori alisema Kampuni ya Romario ya Dubai yenye tawi hapa nchini itatoa vifaa vya mazoezi na mechi.

"Mkataba hu utakuwa na faida kwetu mwaka jana tulikuwa tukitoa Sh 120 milioni kwa kununua vifaa vya mazoezi na mechi kama jezi, mipira bipsi na vitu vingine.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Romario, Minhaal Dewji alisema vifaa hivyo vina ubora na imara zaidi, hivyo ana matumaini Simba itapata manufaa.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz