Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Jezi Yanga zaanza kulipa

69559 Jezi+yanga+picha

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

SAA chache baada ya uzinduzi mpya wa jezi za Yanga msimu wa mwaka 2019/20 tayari imeshaiingizia milioni moja klabu hiyo baada ya wanachama wawili kununua jezi hizo.

Yanga imezindua jezi zake leo na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Abas Tarimba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa klabu hiyo Lucas Mashauri wamenunua jezi hiyo kwa laki tano kila mmoja.

Jezi mbili za klabu ya Yanga leo katika uzinzuzi huo zimeingiza Sh 1 milioni baada ya Tarimba na Mashauri kununua kwa bei hiyo, huku matarajio ya uongozi kuvuna mapato zaidi kupitia mradi huo.

"Kama ni kuiga tunaiga walio endelea Yanga wameiga watu wa ulaya ambako mpira ndio umeendelea, nilikuwa nazitamani hizi jezi niki tayali kutoa laki tano nimeze kupata hii jezoi rangi ya manjano nimeipenda sana," alisema Tarimba na kuongeza;

"Nimeshawahi kuona jezi nyingi sana hii jezi ni bora watanzania tuisapoti klabu yetu ya Yanga, tuachane na tabia za kununua jezi chini ya miti ukitaka jezi imara nunua chini ya kampuni ya GSM," alisema Tarimba.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk Msolla alifichua mashabiki na wanayanga walikuwa wakikwepa kununua jezi za klabu yao kwa kutambua kuwa hazikuwa zikiinufaisha klabu, lakini walichokuja nacho kwa sasa kitafanya Jangwani wanufaike na jezi zenye nembo zao.

Chanzo: mwananchi.co.tz