Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Filamu ya Kakolanya, Yanga sasa ipo hivi

39336 Beno+pic VIDEO: Filamu ya Kakolanya, Yanga sasa ipo hivi

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

ILE filamu ya kipa Beno Kakolanya na mabosi wake Jangwani, inaelekea mwishoni baada ya pande mbili kufikia hatua ya kuachana, huku Yanga wakisisitiza wanasubiri kuteta na wanasheria wao kabla ya kutoa maamuzi ya mwisho.

Kakolanya aliyejiweka kando baada ya kudai malimbikizo ya mishahara yake pamoja na pesa zake za usajili, hali iliyofanya kocha Mwinyi Zahera kumwondoa kwenye mipango yake, lakini baada ya kuzungushana kwa muda mrefu, kipa huyo ameandika barua Jangwani kuomba kuvunjiwa mkataba

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kana na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay kwamba Kakolanya ameandikia barua kupitia kwa Mwanasheria wake Leonard Richard kuomba avunjiwe mkataba baada ya klabu hiyo kushindwa kutimiza baadhi ya vipengele vya mkataba.

Mwanasheria huyo alikaririwa na Mwanaspoti kwamba mteja wake aliingiziwa pesa za mishahara yake ambayo ilidaiwa ni kutokana na miezi aliyofanyakazi yake. Lakini jana Jumatano, Lukumay alisema walimuingizia pesa za mishahara mchezaji huyo kama wachezaji wengine wanavyotakiwa kupata.

“Beno ni mchezaji wetu na alisaini mkataba wa miaka miwili, mkasa wake ulianzia tangu tunaenda kucheza Mwadui baada ya yeye na Kelvin (Yondani) kushindwa kujiunga na wenzake, hata hivyo Yondani alitaja sababu za kushindwa kujiunga na wenzake lakini Kakolanya imekuwa tofauti,” alisema.

Lukumay aliongeza kupitia mwanasheria wa mchezaji huyo wamepokea barua ya kutaka kuvunja mkataba, lakini watakaa kwanza na Wanasheria wa klabu hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz