Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Dar yasimama mechi ya Yanga vs Simba

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hali halisi inayoendelea Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mashabiki wanaendelea kuingia uwanjani kwa ajili ya kuzishuhudia timu zao kwa maana ya Yanga kuwa wenyeji wa Simba katika mechi inayopigwa saa 10:00 jioni.

Ni mechi ya mzunguko pili baada ya raundi ya kwanza timu hizo kutoshana nguvu.

Shamrashamra ni za kawaida kutokana  na mashabiki wanaoshangilia na ngoma bado hawajafika kukinukisha.

Hali ya usalama kwa maana ya Jeshi la Polisi wao wamefika mapema huku wakionekana wakitimiza wajibu wao wa kusimamia usalama wa raia pamoja na kuwaelekeza maeneo ya kukaa.

Unaonekana ni mchezo mgumu ambao mashabiki wanasubiri nani zaidi ndani ya dakika 90.

Staa wa zamani wa Simba, amesema kama Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi wakitulia na kufanya umakini katika safu yao basi Yanga watapigwa 7-0.

Mgosi anasema hakuna cha ushirikina bali anazungumzia kiufundi namna ambavyo Simba wapo vizuri kwa mchezaji mmoja mmoja akidai tofauti na Yanga.

Anasema mara nyingi kinachowaangusha Simba ni wachezaji kuvimba vichwa wakisahau Yanga watakuwa wanahitaji heshima mtaani.

"Simba kiufundi ipo vizuri ukilinganisha na Yanga kwa mechi zao tatu za mwisho lakini kwa kuwa ni watani basi lazima Kagere, Okwi na Bocco wafanye kweli.

"Jambo lingine ambalo ni tatizo kwa Simba na Yanga ni viwango vya wacheza ni unavyomuona leo sivyo anavyokuwa kesho pia sio watu wa kulinda uwezo wao.

"Lakini pia lazima mwanafamilia wa soka wajue wazi kwamba kuna matokeo ya aina tatu kufungwa, ushindi na sare kwani pande zote mbili zinataka kucheka," anasema Mgosi.

 

Vilevile benchi la ufundi la Yanga limemrudisha kikosi cha kwanza beki Kelvin Yondani katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania aliingia kutokea benchi.

Beki huyo pamoja na mwenzake Andrew Vincent wamekuwa hawachezi pamoja katika mechi za Yanga za hivi karibuni, lakini leo wameanza pamoja kwenye kikosi cha kwanza.

Mrisho Ngassa ambaye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo mwaka jana alikosekana kwenye kikosi cha kwanza, ameanzia benchi kwa mara nyingine leo.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo kipa Ramadhani Kabwili atakayesaidiwa na mabeki Yondani, Andrew Vincent, Gadiel Michael na Paul Godfrey 'Boxer'

Viungo ni Ibrahim Ajibu, Feisal Salum, Papy Tshishimbi na Abdallah Shaibu 'Ninja' wakati washambuliaji ni Amissi Tambwe na Heritier Makambo.

Kwa upande wa Simba kikosi  chao, Aish Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Clatous Chama, Jonas Mkude, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.



Chanzo: mwananchi.co.tz