Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO : Bodi Ligi yailima faini Yanga, kuja na kanuni kali zaidi

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bodi ya Ligi imeitoza faini klabu ya Yanga kufuatia makosa mawili ya uvunjifu wa kanuni katika mchezo dhidi ya KMC.

Mtendaji Mkuu wa Bodi, Boniface Wambura amesema Yanga ilifanya makosa mawili ya kutoingia vyumbani na kupita mlango ambao hawakustahili walipokutana na KMC mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wambura amesema kwa makosa hayo ya Yanga kwa kila kosa imetozwa kiasi cha Sh 3 milioni ikiwa ni adhabu ya kiwango cha mwisho.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Steven Mnguto na pia ndiyo mwenyekiti wa kamati ya saa 72 iliyotoa uamuzi hayo amesema Yanga imekuwa ikiendelea kufanya makosa hayo na kuipelekea bodi yao kutumia kiwango cha mwisho cha adhabu.

Aidha Mnguto amesema kutokana na mapungufu ya udhaifu wa kanuni zao msimu ujao watahakikisha wanaunda kanuni kali zitakazokomesha makosa hayo ya mara kwa mara.

Amewataka klabu ya Yanga kupitia viongozi wao kujitathimini katika makosa hayo kwani yanainyima klabu yao fedha ambazo zinakatws katika mapato yao.



Chanzo: mwananchi.co.tz