Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Aussems: Al Ahly, Vita hapa Dar patachimbika

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema alijua itakuwa vigumu kwao kupata pointi dhidi ya Al Ahly na AS Vita ila bado nafasi ya kusonga mbele ipo.

Akizungumza baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Aussems alisema amebakiwa na mechi tatu kati ya hizo mbili atakuwa nyumbani hiyo ni faida kwao.

Simba mechi zake mbili za nyumbani ni dhidi ya Al Ahly na AS Vita kabla ya kwenda Algeria kumaliza dhidi ya JS Saoura.

“Hakuna linaloshindikana katika mpira tuliwafunga Saoura 3-0 hapa, na wao wamepata sare mbili dhidi ya Al Ahly na AS Vita kila kitu kinawezekana.”

"Tumezifutilia timu zote tatu ambazo tumecheza nazo na tunafahamu ugumu, ubora na udhaifu wa timu hizo ambazo tumepanga kushindana nazo kadri tunavyoweza ili kufikia malengo ya timu," alisema Aussems.

"Tumesahau matokeo ya mechi iliyopita na tunafahamu kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Simba na Al Ahly ambao ni timu kubwa Afrika hata AS Vita ni hivyo hivyo kwahiyo hata mawazo si makubwa kwani tulipoteza dhidi ya klabu kubwa ambazo zimecheza fainali za mashindano makubwa msimu uliopita.

Simba watacheza mechi ya marudiano na Al Ahly Jumanne Februari 12, lakini kabla ya kukutana na hao watacheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui Alhamisi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema hawakutarajia kufungwa katika mchezo huo walijiandaa kushinda sasa wamesahau matokeo hayo wanaangalia michezo iliyobaki.

Alisema nafasi katika kundi lao bado ipo na wataendelea kujipanga zaidi kuhakikishana wao wanapata ushindi katika michezo yao ya nyumbani na hilo linawezekana baada ya kuumizwa na walichokipata.

"Kila mmoja kaumizwa na matokeo hayo, tumekaa pamoja na wachezaji wameonyesha kuumizwa na matokeo na wameweka wazi kuwa hawatakubali kuona wanafungwa tena katika uwanja wa nyumbani," alisema Magori.

Nahodha wa Simba, Haruna Niyonzima alisema matokeo waliyoyapata sasa yamebaki ni historia na kuweka wazi kuwa hataki kuzungumzia suala la hali ya hewa wamekubali matokeo wanaangalia michezo mingine.

"Tumebakiwa na nafasi mbili ambazo ni muhimu sana kwetu za michezo ya nyumbani tukizitumia vizuri tunaweza tukajitengenezea nafasi ya kuingia hatua inayoifuata," alisema Niyonzima.



Chanzo: mwananchi.co.tz