Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalendo wamshinda bosi wa timu, aingia uwanjani na bastola

4631 4A19EA6300000578 5488719 PAOK Chairman Ivan Savvidis Walked Onto The Field Carrying A Gun M 176 TZW

Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mmiliki wa klabu ya PAOK inayoshiriki ligi kuu nchini Ugiriki (Greek Super League), Ivan Savvidis amejikuta akishindwa na uvumilivu na kuingia uwanjani na bastola huku akimuambia mwamuzi umekwisha  baada ya kuchelewa kuamuru bao lao lililopatikana katika mchezo wao  dhidi ya timu ya AEK .



Katika mchezo huo uliyopigwa jana siku ya Jumapili mchezaji wa PAOK, Fernando Varela aliipatia bao timu yake dakika za mwisho kwa jitihada binafsi kisha mwamuzi akachelewa kuamuru kuwa goli hali iliyopelekea mmiliki wa timu hiyo, Ivan Savvidis kupandwa na jazba  na kuingia uwanjani huku akiwa na bastola kiunoni.



Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo meneja wa klabu ya AEK, Mhispania, Manolo Jimenez amesema kuwa hawakufahamu kuwa alikuwa na bastola ni ghafla tu wameiyona akiwa nayo na kumuambia mwamuzi umekwisha.



Msimamo wa ligi kuu ya Ugiriki huku PAOK wakishika nafasi ya tatu na alama zao 50 wakati ya kwanza ikishikwa na hasimu wake huyo AEK mwenye pointi 55.

Chanzo: bongo5.com