Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja waipa Simba mbinu mpya vs Prisons

55761 SIMBA+PC.png

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Kocha Patrick Aussems anajua kubadilika kama kinyonga anapoona mambo hayaendi katika njia yake ya kusaka ubingwa wa pili mfululizo kwa timu yake Simba msimu huu.

Na hilo lilithibitika katika mechi iliyopita ya Simba dhidi ya Mbeya City ambayo Wekundu wa Msimbazi walisubiri hadi dakika za lalasalama kupata bao la ushindi wa 2-1 kwenye uwanja uliojaa maji na tope wa Sokoine jijini hapa.

Mbelgiji huyo aliwaambia wachezaji wake wabadilishe staili ya uchezaji wakati wa mapumziko, vinginevyo mambo yangeharibika, amebainisha beki mkongwe wa timu hiyo, Erasto Nyoni.

Nyoni ambaye alianzia benchi katika mechi hiyo ambayo Simba walitangulia kufungwa kupitia goli la Idd Seleman ‘Naldo’ lililowaweka wenyeji Mbeya City mbele hadi wakati wa mapumziko, alisema mbinu walizopewa katika vyumba vya kuvalia ndizo zilizopindua matokeo.

Alisema baada ya mechi hiyo ambayo Simba walionekana kukaribia kudondosha pointi kabla ya Jonas Mkude kusawazisha katika dakika ya 68 na Meddie Kagere kufunga la ushindi dakika tano kabla mchezo kumalizika, Simba sasa iko tayari kukabili changamoto za Uwanja wa Sokoine na wamedhamiria kuondoka na pointi sita zote za mjini humo.

“Tunajua hii ni hali ambayo hatuwezi kuikwepa, lakini tunachoweza kuwahakikishia mashabiki wa Simba ni kwamba, lazima tutakomaa kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi,” alisema Nyoni.

Simba wataikabili Tanzania Prisons leo kwenye uwanja huo wa Sokoine, huku mashabiki wa klabu hiyo wakiwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi.

Naye kocha mkuu wa maafande Tanzania Prisons, Adolf Rishard amesema anatambua ugumu wa mechi ya leo dhidi ya Simba lakini hana hofu yoyote kwani ana imani vijana wake wataifunga Simba.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo alisema wanafahamu kiwango ilichonacho Simba kwa sasa, lakini vijana wake wapo vizuri na wana shauku kubwa kushinda.

“Niwatoe hofu mashabiki na wapenzi wa Prisons, wapo waliodhani tukio la sisi kupata ajali wakati tunarejea jijini hapa (Mbeya) baada ya mechi na Yanga linaweza kututoa kwenye ari ya mchezo wa kesho (leo) hapana tupo vizuri, vijana wangu wapo vizuri zaidi.

“Tunataka kuleta heshima kwenye uwanja wa nyumbani, hatuwahofii kwa chochote hao Simba. Na juzi mimi na wachezaji wangu tulikuwapo pale Sokoine kuwatazama wakati wanacheza dhidi ya Mbeya City, tuliona upungufu wao na tutautumia kuwafunga”.

POVU LA MANARA

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameomba viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kukemea tuhuma zinatolewa na baadhi ya makocha ambao wamekuwa wakituhumu shirikisho hilo na Bodi ya Ligi kuwabeba Simba ili watwae ubingwa wa msimu huu.



Chanzo: mwananchi.co.tz