Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

“Uwanja mbovu soka bovu”- Wadau wa soka wafunguka (+Video)

1114 Capture 9 TZW

Fri, 5 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Katika harakati za kunyanyua mpira wa miguu nchini Tanzania Kampuni ya kubashiri ya SportPesa imewatengeneza wataalamu ambao ni wazawa wakutengeneza (Pitch) nzuri za viwanja vya mpira wa miguu.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba leo alhamisi jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Tarimba amesema ili mpira wetu ukue ni lazima tuwe na viwanja vizuri kwani uwanja ukiwa mbovu usitegemee kuwa na timu yenye uwezo mkubwa.

Kwa upande mwingine Tarimba ameiomba serikali na timu za soka kuchangamkia wataalamu hao kuwatumia katika kurekebisha viwanja vyao ili waweze kuwa na viwanja vya kisasa kama ulivyo uwanja wa Taifa. Tazama video yake hapa chini

 

 

Chanzo: bongo5.com