Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uturuki yaitekenya Serengeti Boys mabao 5-0

45612 Pic+serengeti Uturuki yaitekenya Serengeti Boys mabao 5-0

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya Taifa ya Taifa ya  vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania'Serengeti  Boys' imechapwa mabao 5-0 na wenyeji  Uturuki katika michuano ya UEFA Assist inayofanyika nchini humo.

 Huo unakuwa mchezo wa pili Serengeti Boys kupoteza katika michuano hiyo baada ya ule wa kwanza kufungwa na Guinea bao 1-0  huku mchezo wa pili wakiibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Australia .

Serengeti Boys ilionekana kucheza kwa kiwango cha  kawaida katika mchezo huo huku safu ya kiungo ikionekana kushindwa kuleta muunganiko mzuri na washambuliaji.

Washambuliaji wa Serengeti Boys wakiongozwa na  Kelvin John walionekana kushindwa kufanya maamuzi  pindi wanapolifikia lango la wapinzani wao na kujikuta wakipiga chenga zisizo na  faida na mwisho kupokonywa mipira.

Serengeti Boys ilipangwa Kundi A katika michuano hiyo pamoja na  wenyeji Uturuki,Guinea na Australia  wakati kundi B lina timu za lCameroon, Uganda, Morocco na Belarus na Kundi C lina timu za Senegal, Nigeria, Angola na Montenegro.

Tanzania inatumia michuano hiyo  kwa ajili ya kujiandaa na Fainali za   Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana chini ya umri wa miaka 17   ambayo yatafanyika hapa nchini kuanzia April 14 hadi 28 jijini Dar es Salaam.



Chanzo: mwananchi.co.tz