Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata waibuka kudukuliwa akaunti za Instagram za Maulid Kitenge

KITENGE.png?fit=656%2C424 Maulid Kitenge

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Baada ya kuwepo kwa sintofahamu juu ya akaunti za Mtangazaji nguli wa habari za michezo nchini Tanzania ndugu Maulid Kitenge na kuwa hazipatikani kweye mtandao wa Instagram mapema asubuhi ya leo ameweka wazi kila kitu kuhusu akaunti hizo na kusema zimechukuliwa.

Akizungumza katika moja ya mahojiano yake aliyofanya asubuhi ya leo katika kituo cha habari ambacho anakifanyia kazi kwasasa Kitenge amesema baada ya kuanza mchakato wa kurudi kwenye kituo chake hicho cha awali  akaunti zake mbili za instagram zilichukuliwa.

Aidha kitenge ameongeza kwa kusema  kuwa hajatendewa haki kwani akaunti hizo ni sehemu nyingine anayotumia kupata riziki, ” mimi sijui ni nani amefanya kitendo hicho, nasikia watu wengi wakihusisha watu lakini mimi sijui ni nani amefanya hivyo ”

Hata hivyo kitenge amebainisha kuwa kwasasa hana akaunti Instagram na ahadi kuziridisha akaunti hizo.

Mtangazaji Maulid Kitenge amerudi EFM baada ya kuachana na kituo cha redio cha WasafiFm alichokuwa anafanyia kazi.

Chanzo: zanzibar24.co.tz