Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utastaajabu fedha anayotumia Mayweather kubadilisha oil ya gari yake

Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Yaani ukitaka kumiliki vitu vizuri basi lazima ujipange kuvitunza na hii inadhihirishwa na Mwanamasumbwi, Floyd Mayweather ambaye ni moja ya wanamichezo wanaomiliki magari ya kifahari duniani.



Kwa mujibu wa mtu wa karibu anayemuuzia magari ya kifahari Mayweather aitwaye Obi Okeke kupitia mtandao wa TMZ amesema Mayweather anatumia dola $25,000 ambayo ni sawa na Tsh milioni 56 kila mwezi kubadilisha oil ya gari lake moja aina ya Bugatti Veyron.

Okeke amesema gari hiyo ambayo ndio gari yake ya thamani zaidi amelinunua kwa Dola milioni 3.3 sawa na Tsh bilioni 7 .

Mwezi Januari mwaka huu Mayweather alitumia zaidi ya milioni 100 kufanyia matengenezo Bugatti yake.

Chanzo: bongo5.com