Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiyoyajua kuhusu Kombe la Carabao, Samatta kuwania taji la kwanza

93625 Pic+samatta Usiyoyajua kuhusu Kombe la Carabao, Samatta kuwania taji la kwanza

Thu, 30 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Mbwana Samatta atakuwa akiwania taji lake la kwanza England wakati klabu yake ya Aston Villa itakapocheza fainali ya Kombe la Carabao Jumapili Machi Mosi kwenye Uwanja wa Wembley.

Mechi hiyo itachezwa 12:30 jioni kwa saa Tanzania, mchezo huo utawakutanisha Aston Villa dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City au Manchester United watakaocheza nusu fainali ya pili leo usiku.

Mechi hiyo itaonyeshwa moja kwa moja na Sky Sports, wakati Villa wakirudi kwa mara ya pili katika uwanja huo wa taifa.

Kila timu itakayofanikiwa kuingia katika fainali hiyo itapewa tiketi 30,000 kwa mashabiki wake huku tiketi 30,000 zilizobaki zitapabaki kwa EFL.

Timu itakayoshinda ubingwa wa Kombe la Carabao itapokea kitita cha pauni 100,000 mshindi wa pili 50,000, pia bingwa anafuzu moja kwa moja kuingia katika raundi ya pili ya Europa Ligi.

Manchester City imetwaa Kombe la Carabao mara sita huku mara moja ikimaliza nafasi ya pili, imefuzu mara tatu katika fainali hizo.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Villa pia imekuwa na rekodi nzuri katika mashindano haya ikiwa imetwaa ubingwa huo mara tano, mara ya mwisho ilipotwaa ubingwa huo ulikuwa msimu wa 1995-96, na hiyo ilikuwa ni mara ya mwisho kwa Villa kutwaa ubingwa wa mashindano.

Mshambuliaji Samatta amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza fainali ya Carabao baada ya Aston Villa kuichapa Leicester City kwa mabao 2-1 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla 3-2.

Ushindi huo unaifanya Villa pamoja na Samatta sasa kusubiri mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili itakayochezwa leo kati Manchester City dhidi Manchester United.

Katika mchezo huo Samatta akicheza mechi yake ya kwanza alifunga bao lakini mwamuzi alikataa akidai ameotea kabla ya kutolewa katika dakika 64 ya mchezo.

Wenyeji Aston Villa walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Targett dakika 22, Trezeguet alifunga bao la pili dakika 90+3, huku bao la kufutia machozi la Leicester City likifungwa na Iheanacho.

Katika mchezo huo macho ya watanzania wengi yalikuwa kwa Samatta ambaye alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza tangu amejiunga na Villa akitokea Genk ya Ubelgiji.

Samatta alijitahidi kuonyesha uwezo wake, lakini alikosa nafasi kadhaa za kufunga katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali.

Chanzo: mwananchi.co.tz