Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushindi Azam waipa presha Yanga

2414ab586ad1917ce3ad8a59bab70557.jpeg Ushindi Azam waipa presha Yanga

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika mchezo uliopigwa kwebye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yaliwekwa kimiani na Prince Dube katika dakika ya 11 na Aggrey Morris dakika ya 90 wakati la KMC bao lao la kufutia machozi lilipachikwa na Abdul Hilary katika dakika ya 41.

Kwa ushindi huo, Azam FC imefikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 29, lakini inaendelea kuwa katika nafasi tatu ikiziwa pointi moja na Yanga iliyopo katika nafasi ya pili baada ya juzi yenyewe kutoka suluhu dhidi ya Namungo mjini Lindi.

Ushindi wa Azam unazidi kuipa presha Yanga katika mbio za ubingwa au kumaliza katika nafasi mbili za kwana huku Simba ikiendelea kuwa kileleni licha ya kutocheza Ligi Kuu mwishoni mwa wiki baada ya kuwa na kibarua cha kimataifa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz