Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa Ajibu ulilenga kujibu pigo la Niyonzima-5

79969 Ajibu+pic

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

JANA Jumamosi katika mfululizo wa makala za aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, tuliona jinsi alivyozungumzia ujio wa Kocha Mwinyi Zahera ulivyowagawa wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo. Katika mfululizo huo, leo anazungumzia lengo la usajili wa kiungo wa zamani wa Simba, Haruna Niyonzima.

Kipi kilikwamisha usajili wa Ilamfya

“Hili nalo ni kama vile niliv yokuambia, unajua Yanga tuna utaratibu wa kila mechi tunayocheza tunafuatilia wachezaji wa timu pinzani, tulikuwa na kundi la ufundi ambalo kama tukiona mchezaji mzuri tunampeleka humo na kumjadili.

“Tulimuona Ilamfya (Charles) wakati huo akiwa Mwadui, kundi la ufundi likamkubali na bahati nzuri (Kocha Mwinyi) Zahera naye alimkubali na akasema asajiliwe haraka, kumbe mchezaji mwenyewe naye alikuwa anataka kuondoka katika klabu yake wakisigana katika mambo ya malipo na kesi ilikuwa TFF.

“Alivyokuja Dar akawasiliana na kocha na kocha akatujulisha kuwa mchezaji amekuja hapa Dar katika kesi yake na tukaonana naye nikiwa na marehemu Urungo tukaongea naye.

“Baada ya maongezi yetu ya mchezaji tulitakiwa kuonana na mtu aliyemtaja kuwa ni meneja wake na nikamfuata mpaka kwake Boko, sikuwahi kumfuata mtu mwenye kazi kama zile lakini nilikwenda na kuonana naye, yule meneja wake hakusita kutuambia ukweli kwamba anajua mimi ni Yanga na yeye ni shabiki mkubwa wa Simba ndakindaki kwa kuwa ni maslahi ya mchezaji tuongee.

Pia Soma

Advertisement
“Tulikaribia kumalizana na mchezaji lakini tulichokuja kugundua nyuma mchezaji hakuwa na mamlaka ya mwisho kuamua aende wapi na ndani ya hilo kulikuwa na harakati zinafanyika kuhakikisha haji Yanga na hii ni baada ya Simba kuambiwa kila kitu, lakini wao wakawa hawana nafasi ya kusajili winga.

“Kilichofanyika Ilamfya akatafutiwa timu ili tu asijiunge na Yanga, tulikubaliana kesho yake tuonane tukawasubiri sana wenzetu hawakutokea mpaka jioni, ilipofika saa 11 jioni kuna wanachama wetu wakatuambia Ilamfya yuko uwanja wa Uhuru na viongozi wa KMC tukashangaa ikabidi tuondoke na kumfuata huko.

“Tulipofika Uwanja wa Uhuru mechi ya KMC ilikuwa imeisha na kijana alikuwa katikati na viongozi wa serikali wa KMC, tukaona isiwe tabu hata kama mchezaji ni mzuri lakini hana msimamo wa wapi anataka kucheza, lakini baadaye kumbe tayari kuna mchezo mrefu ulishakamilika pale TFF Ilamfya alipokuwa anasubiri barua ya kuvunja mkataba na Mwadui, tayari barua ile ilishakwenda KMC wakifanyiwa wepesi na kigogo mmoja wa TFF ambaye ni Simba, kwa hiyo - hiyo ndiyo picha halisi ilivyokuwa na watu wakumbuke kuhusu maslahi mchezaji alishakubaliana kila kitu mpaka utayari wa kuchukua Sh10 milioni ila akazidiwa nguvu.

“Nafikiri haya yote yalifanyika kwa makusudi kuhakikisha Yanga haiimariki hasa kama mnavyofahamu wakati huo Zahera alikuwa anasisitiza sana kuhitaji winga mwenye kasi, sasa hawa jamaa wa upande wa pili wakaona kama angekuja kwetu uimara wetu ungeongezeka.”

Usajili wa Ajibu kumbe ni Niyonzima

Moja ya silaha kubwa ya Yanga katika misimu miwili iliyopita hasa msimu uliopita ilikuwa ni mchezaji fundi Ibrahim Ajibu. Hapa Nyika ambaye alisimamia usajili huo anaelezea kwa nini walimkimbilia nyota huyo.

“Ndiyo, ni kweli kamati yangu ndio ilimsajili Ajibu, nakumbuka tulikuwa tunampigia hesabu muda mrefu kutokana na yeye mwenyewe kuwa na utayari.

“Yanga baada ya kumpoteza Haruna Niyonzima kwenda Simba tulikutana na kamati yangu na kujadili tutafanya kipi ili kuzima kelele za hawa jamaa zetu, kama mnavyojua hizi klabu mbili zina tamaduni zake.

“Baada ya kuona Haruna anaondoka na tulikuja kujua baadaye kwamba alishamalizana na Simba muda mrefu na maongezi yetu hata kama tungesema tutampa benki asingeweza kubaki, tukasema lazima tutafute mtu wa kuziba nafasi yake.

“Jina la Ajibu lilikuwa mezani kwetu na wakati huo alikuwa hataki kubaki katika klabu aliyokuwa, tukawashirikisha makocha wakasema aletwe lakini hao walijadili kiufundi ila na sisi tulisema lazima tulete mtu ambaye atawaumiza Simba.

Nakumbuka mara ya kwanza nilimfuata Ilala kwao na alipotukubalia kuanza mazungumzo nikarudi kwa Sanga (Clement), akaniambia yeye kama kaimu mwenyekiti wa klabu, akaunti ya timu haina fedha lakini Ajibu kama kuna ‘vurugu’ tunaweza kufanya, basi ifanyike asajiliwe.

“Nikaumiza kichwa ikabidi nirudi kwa Seif Magari, BinKleb, marehemu Urungo, Majid na Ndama ambaye alikuwa katika kazi zake akakubali kuahirisha, akaja ndani ya dakika 20 tukakutana. Tulipokutna tukakubaliana kila kitu juu ya maslahi ya mchezaji, baada ya hapo tukamuita tulipokuwa akaja, tukamalizana naye na kwa kuwa hakutupa usumbufu wakati wa kumsajili mwenzetu mmoja akafurahi akampa gari aina ya Toyota Brevis kama zawadi na kisha tukakubaliana wote tunyamaze na yeye arudi klabu aliyokuwa.

“Tukawaacha jamaa zetu wakikimbizana naye kushoto na kulia wakihitaji kumbakiza, lakini sisi wala hatukuwa na muda naye tena tukawaachia wao.

“Tuliamua kunyamaza kutokana na kuwa bado alikuwa amebakiza kama mwezi mkataba wake na Simba kumalizika, tukasema tusijitafutie ubaya na TFF ile siku ambayo Ajibu anatambulishwa pale Jangwani klabuni, ilikuwa kama kucheza na akili za watu kwani muda mrefu alishasaini Yanga na ninachoshukuru Ajibu alicheza Yanga na kuipa mafanikio kuliko Haruna alivyowatumikia jamaa zetu.

ITAENDELEA KESHO JUMATATU.

Chanzo: mwananchi.co.tz