Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umemsikia Madee baada ya Arsenal kutinga fainali

1900 Sequence 01.Still038

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Kikosi cha Chelsea kilichochini ya kocha wake Antonio Conte kimeshindwa kutoka salama katika dimba la Emirates, wakicheza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Ligi, Arsenal ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huo.



Pamoja na kuwa Chelsea walianza kupata goli la mapema dakika ya 7 kupitia kwa Eden Hazard, Arsenal walifanikiwa kusawazisha dakika ya 12 baada ya Rudiger kujifunga, dakika ya 60 ndio ilikuwa mbaya zaidi kwa Chelsea kwani Granit Xhaka alifunga goli la ushindi kwa Arsenal na kuufanya mchezo umalizike kwa 2-1.



Ushindi huo sasa unatoa fursa kwa Arsenal kukutana na Man City katika mchezo wa fainali ya Kombe hilo, mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Wembley, muimbaji wa Bongofleva Madee ambaye anadaiwa kuhuzunishwa na kuondoka kwa Sanchez katika club ya Arsenal anayoishabikia.

Madee ameamua kuandika ujumbe huu kama kejeli kwa wanaoibeza timu yake baada ya Sanchez kuwakimbia “Coyg tumeenda Wembley bila kupita Chile” akimaanisha kwamba Arsenal imefuzu kucheza fainali bila uwepo wa Sanchez ambaye taifa lake ni Chile.



VIDEO: Juma Nyosso alivyokamatwa na polisi baada ya game ya Kagera vs Simba

Chanzo: millardayo.com